Klabu ya Olympique Marseille ya nchini Ufaransa, imekua ya kwanza kuonyesha nia ya kumsajili beki wa kati wa majogoo wa jiji (Liverpool) Mamadou Sakho.

Tayari Sakho ameshafunguliwa mlango wa kutokea na meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, kwa kuambiwa anaweza kuondoka wakati wa majira ya baridi (Mwezi Januari).

Olympique Marseille wanajiandaa kuwasilisha ofa ya usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 26, huku wakipata ushawishi wa kufanya hivyo kutokana na mipango ya muwekezaji kutoka nchini Marekani Frank McCourt.

Sakho alisajiliwa na Liverpool mwaka 2013 akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain, ambao mpaka sasa hawajaonyesha nia ya kutaka kumrejesha Parc des Princes.

Jose Fonte: Sina Mpango Na Man Utd
Cristiano Ronaldo Atafuta Hifadhi Sporting Lisbon