Kuoa au kuolewa ni jambo ambalo sio watu wote wanabahatika kulipia, lakini inapotokea mwanaume ameamua kuoa yapo mambo mengi anayoangalia kwa mwanamke na kufikia hatua ya kuchukua uamuzi na kuoa, japo walimwengu wanasema hakuna jambo gumu na zito kama kukosea kuchagua mume au mke.

Hapa chini nina mambo kadhaa ambayo mwanaume anaweza akawa anayafanya kumchunguza mwanamke aliyenaye kama anafaa kuwa mke, japo siku hizi mambo yamebadilika wanaume wamekuwa wakiangalia sura, umbo, rangi, pesa na kadhalika jambo lililopelekea ndoa nyingi kuvunjika na kutodumu.

Kama ambavyo tumeona ndoa za mastaa mbalimbali kuvunjika, haya hapa ni baadhi ya mambo ambayo mwanaume anaweza kumtegea mwanamke kumpima kama anafaa kuwa mke.

1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa.

2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakujaribu aone kama utasema “Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu”.

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate ‘dinner’ usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakujaribu aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Upo chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa ‘out’ halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama yake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkitoka . Anakuomba ushauri afanyaje, Wewe unamwambia “Baby twende out” , suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia”. Woiyeeee! ‘My sista ‘hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!.

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? ‘My sister’, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada, Sio tu wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalau akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.

9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hautaona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia zawadi ndogo ndogo. ‘Sometimes’ unakuja na ‘boksa’ au kavesti au ‘kadodoranti’. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia.

Video: Kinana, Makamba sasa shubiri CCM, Diwani CCM alivyonaswa na rushwa
Kesi za matunzo ya watoto zaongezeka Tanga

Comments

comments