Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, leo amewasilisha rasmi Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/17, ikiwa ni bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli.

Katika Bajeti hiyo yenye shilingi trilioni 29.5, matumizi kawaida yametengewa shilingi trilioni 17.19 na shilingi trilioni 11.82 kwa ajili ya maendeleo.

Haya ni mambo 26 muhimu unayopaswa kuyafahamu kuhusu Bajeti hiyo iliyosomwa leo Bungeni:

  1. Serikali imetenga shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya uanzishwaji wa mahakama ya ufisadi
  2. Zabuni zote za matangazo, vyakula, usafiri, promotion n.k, zipewe kipaumbele kwa taasisi za serikali pekee.
  3. Riba ya mikopo kwenye mabenki kuongezeka.
  4. Mzabuni yeyote asiye na mashine za EFD hatapata zabuni serikalini isipokuwa kama ana uthibitisho wa kuruhusiwa na tra.
  5. Mikutano, makongamano, semina, zote zisifanyikie kwenye kumbi za starehe bali kwenye kumbi za Serikali.
  6. Vinywaji vikali,vinywaji visivyo na vilevi, mvinyo,bei juu.
  7. Sigara zote ushuru juu.
  8. Maji ya ndani hakuna ongezeko.
  9. Ushuru wa mafuta ya kulainisha mafuta bei juu.
  10. Ushuru wa gesi juu.
  11. Ushuru wa samani zote zinazotengenezwa nje ya nchi bei juu.
  12. Utengenezwaji wa mufuko ya plastick yenye ukubwa wa microwaves bei juu.
  13. Ushuru wa bidhaa kutoka nje bei juu.
  14. Msamaha wa kodi za mapato kwa malipo ya kiinua mgongo kwa wabunge yanayolipwa kila baada ya miaka mitano umefutwa.
  15. Mapato yote tanayotokana na hisa kwenye makampuni sasa kutozwa kodi.
  16. Kodi ya mapato ya mshahara (PAYE) kupungua kutoka asilimia kumi a moja mpaka 9.
  17. Mapato ya pango katika mifuko ya jamii sasa kutozwa kodi.

19. Tozo ya kuendeleza mafunzo ya ufundi stadi, kupunguzwa.

20. Kodi ya usajili wa uhamisho wa umiliki wa gari kutoka laki moja na nusu mpaka laki mbili.

21.Kodi ya namba binafsi ya magari sasa shilingi milioni kumi.

22.Ushuru wa forodha juu kwa mpaka asilimia kumi kutoka moja kwa bidhaa za chuma.

23.Bidhaa za chuma zinazotumika katika ujenzi wa madaraja zaondolewa ushuru.

24.Misamaha ya kodi kwa taasisi za dini,inapendekezwa kufutwa,taasisi za dini zitalazimika kulipa kodi.na kama kuna haja ya msamaha,ibidi taasisi za dini ziombe msamaha ama kurudishiwa.

  1. Petrol,disel na mafuta ya taa ,ushuru wa barabara utabaki kama ilivyo sasa.
  2. Kodiza ushuru wa forodha kwenye maduka ndani ya majeshi ya ulinzi na usalama umeondolewa,umesitishwa.Ila kwa wanajeshi na askari watakuwa wakipewa posho,uondolewaji wa msamaha huu wa kodi kwenye maduka ya majeshi umelenga kuwadhibiti wale wajanja waliokuwa wanatumia fursa hiyo.
  3. Serikali kununua ndege 3 kwa ajili ya Shirika la Ndege Nchini (Air Tanzania).
  4. Mapato yote ya halmashauri na taasisi ya umma sasa kuwekwa Hazina Kuu.

Credit: Dotto Bulendu

TFF Yaanza Kutoa Fomu Za Leseni Kwa Klabu
Naibu Spika awavuruga wabunge wa Ukawa, Aagiza wasilipwe Posho wakisusa