Maji ni muhimu sana katika mwili wa binadamu, yanahitajika kwa zaidi ya asilimia 60 katika mwili. Shirika la Afya Duniani (WHO) linaonesha kuwa idadi ya watu kunywa maji duniani imeongezeka kutoka asilimia 76 mwaka 1990 mpaka kufikia asilimia 91 kwa mwaka 2015.
 
Niwazi kwamba kiwango cha unywaji wa maji kinatofautiana baina ya mtu na mtu. Aidha inashauriwa kwa siku mtu kunywa zaidi ya lita mbili za maji kiafya kwani binadamu hupoteza maji mengi kwa kutoka jasho na mkojo.
Dar 24 leo inakufahamisha dalili zitakazokuonyesha kiwango chako cha unywaji wa maji, kama unakunywa maji ya kutosha au haunywi maji ya kutosha.
  • Kupungua kwa kiwango cha mkojo

Kiafya mtu anatakiwa kwa wastani akojoe mara 6 hadi saba kwa siku. Kama unakojoa chini ya mara mbili kwa siku basi gundua hunywi maji ya kutosha.

  • Ngozi kuwa kavu sana

Ukiona una ngozi kavu basi tambua huna maji ya kutosha mwilini kwani ata kiwango cha maji kwenye ngozi yako inatokana na unywaji wako wa maji..

  • Kuumwa kichwa

Ukiona unasumbuliwa sana na kichwa basi tambua kichwa hicho kinawezekana kua ni sababu ya upungufu wa maji.

  •  Mdomo mkavu

Ukosefu wa mate na mdomo kuwa mkavu hiyo husababishwa na upungufu wa maji.

  •  Rangi ya mkojo

Rangi ya mkojo inatakiwa iwe nyeupe ikiwa na unjano kwa mbali kama unakunywa maji ya kutosha. Kama ukiona rangi ya mkojo si ya kawaida kuwa njano kupitiliza basi tambua una upungufu wa maji mwilini.

Zifahamu Mbinu Chafu Na Sababu Za Rafiki Msaliti Kumchukua Mpenzi Wako

Hata hivyo Dkt. Thomas Mboya kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema kuwa mbali na dalili izo pia kuna dalili nyingine kama mtu kupata kizunguzungu, kutotokwa na jasho hata kipindi cha joto, kutokwa na haja kubwa ngumu na ngozi kujikunja.

Naye Dkt. Mariam Maroa kutoka hospitali ya wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam anasema maji ni umuhimu katika mwili wa binadamu kama vile kusaidia katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, mfumo wa damu, na kuweka hali ya jotomwili sawa.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF, watu bilioni 1.1 hawana uwezo wa kupata maji safi duniani. Hii inaweza kuwa sababu ya watu kutokunywa maji kwa kiwango kilichowekwa kwa mujibu wa afya.

Kunywa maji kwa Afya.

Wananchi Pwani washauriwa kushirikiana katika masuala ya kijamii
Serikali kujenga kivuko cha juu kawe bondeni