Katika mahusiano yapo mengi ambayo ukiyafanya yanaweza kuwa chukizo kwa mwanaume au mwanamke, ila kila jinsi ina namna ambavyo imeumbwa, kuna baadhi ya mambo wanawake hawayapendi kwa wanaume pia yapo mambo ambayo wanaume hawayapendi kwa wanawake ambayo yanaweza kuwa chanzo namba moja cha kuvunja uhusiano na mpenzi wako bila kujali ni muda gani mmedumu katika penzi hilo.

Leo tuyazungumzie yale ambayo wanaume hawayapendi kutoka kwa wanawake, kama kuna mwanamke anaangukia katika kundi moja wapo ajue dhahili kuwa mwanaume wake hafurahishwi naye.

Na ndio sababu wanaume wengi huchepuka endapo atakutana na mwanamke mwenye sifa hizi;

Muongeaji sana
Mwanamke muongeaji sana asiyekuwa na staha, mwanamke ambaye hawezi kumvumilia mwanaume pale anapokuwa akimsema kwa jambo f’lani kwa nia ya kutaka maelewano ni tatizo.

Namzungumzia yule ambaye muda wote anataka kushindana na mume/ mpenzi wake katika kuongea, yaani kuonesha kuwa hajakosea, anaonewa au na yeye yumo kwenye kuongea, huyu hawezi kumshika mtu wake.

Mwanamke anayeijenga ndoa yake anatakiwa kuwa chini pale mwanaume anapokuwa anapaza sauti, akishapoa na wote mmepoa. kama una dukuduku lako ongea naye taratibu.

Haiwezekani mume na mke kuwa juu hasa mnapokuwa kwenye mgogoro, inatakiwa mwanamke kumsoma mume wake au mpenzi wake kwa wakati huo.

Wivu wa kupindukia
Mwanamke mwenye wivu wa kupindukia humfanya mwanaume kukosa amani kwani hata awapo kazini kwake mwanamke atataka kumfuatilia na kumnyima uhuru.

Hawa wenye tatizo hili huachwa na wanaume wao haraka kwani wengi hawapendi kuonewa wivu wa hivyo, wengine huuita wivu wa kijinga.

Kujipamba kupitiliza
Mwanamke kama mwanamke ni mapambo na ili awe mwanamke anao ulazima wa kuhakikisha anaonekana smati kwa kujipamba lakini si kama wafanyavyo wanawake wa siku hizi.

Wanaume wengi wamejikuta wanachukizwa na hali ya mwanamke kujipamba kupitiliza.

Yaani unakuta mwanamke anajipamba utadhani siku hiyo ni siku yake ya kufunga ndoa, hilo ni tatizo na husababisha hata mwanaume kuogopa kuongozana naye.

Sasa je, kama unatoka na mume au mpenzi wako, unajipamba hivyo kumfurahisha nani hasa? Mbona ukiwa nyumbani unakuwa wa kawaida tu?

Matumizi makubwa ya fedha
Mwanamke mwenye matumizi makubwa ya fedha ambaye hafikirii kesho itakuwaje ni adui mkubwa wa mwanaume.

Hata kama atakuwa anakupenda kiasi gani, atakuvumilia siku za mwanzo lakini kadiri mnavyokwenda atajitoa kwako taratibu. Hii ni kwa sababu mwanaume atahisi siku akija kuwa hana kitu anaweza kuibiwa na wenye fedha.

Norwich yaivuruga Man City, yaweka historia
Je unafahamu faida za maharage mwilini? fuatilia hapa