Yapo mambo mengi ambayo wazazi huwaambia watoto wao kwa kuwa wanawapenda sana na wangetaka kuwaona wakiwa na furaha kila mara wakati, lakini baadhi ya maneno hayo hugeuka tatizo kwa watoto hao bila wao kufahamu.

Leo nitazungumzia mambo 10 ambayo wengi hupenda kuwaambia watoto wao kimakosa.

1. Acha tu nitafanya

Inawezekana unampenda sana mwanao na usingependa ahangaike sana anapofanya jambo fulani ambalo unahisi hatalikamilisha kwa ufanisi. Lakini ni kosa kubwa sana kumwambia mtoto “acha nitafanya” kwa kuwa amelalamika baada ya kuhangaika akijaribu. kumbuka uwezo wa mtoto katika jambo fulani hukua kwa haraka pale anapohangaika kulitimiza kwa kuwa ubongo wake hushungulika kwa kila hali. Unachotakiwa kukifanya kama mzazi ni kumuongoza jinsi ya kukitimiza.

2. Usilie !

Wazazi wengi hasa wa kiafrika hufanya kosa hili kwa kuwa tu wanapenda kuwarushia furaha ya haraka watoto wao hasa pale wanapoona wanalia. Lakini wataalam wa saikolojia wanaeleza kuwa wakati mwingine mtoto anapolia huonesha hisia zake za dhati na hilo ni suala la kawaida. Kumwambia mwanao kwa masikitiko kuwa usilie unamtengenezea mazingira ya kujua kuwa kulia ni kitu kibaya. Badala yake unapaswa kumueleza kwa nini asilie wakati huo.

3. Kwa nini usiwe kama ‘fulani’

kids

Utakosea sana unapomuelekeza mwanao kwa kutumia kauli hii. Kwa sababu unampunguzia hali ya kujiamini na kudhani kuwa yeye hana uwezo kama watoto wenzake. Hii humuathiri kisaikolojia anakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uwezo wake. Kauli hizi humfanya mtoto kuwa muoga kudhubutu kuanzisha anapokuwa na wenzake.

Hivyo, anapoteza nafasi ya kujijengea kipaji cha uongozi kwa kuwa anakuwa na mashaka na uwezo wake.

Badala yake unapaswa kumuonesha jinsi ya kufanya vizuri na kumpongeza kwa uwezo wake.

4. Subiri hadi baba/mama yako akirudi

Kauli hii sio nzuri hasa pale mtoto anapokuwa amekosea na unadhani anapaswa kuadhibiwa. Hii inamjenga vibaya mtoto kisaikolojia kwakuwa ataamini kuwa wewe hauna uwezo wa kuchukua maamuzi dhidi yake. Au kumuona baba au mama yake huyo kama ‘nyapara’ kwake. Atakaporudi nyumbani mtoto huyo atakosa amani kwa muda na kuonesha nidhamu ya uonga. Badala yake, chukua hatua au mpe maelekezo yanayostahili.

5. Nakuahidi!

Girl counting  change from piggy bank

Girl counting change from piggy bank

Ahadi ni zaidi ya deni kwa mtoto, hii ni kwa sababu mtoto huamini kuwa baba au mama yake anaweza kufanya vitu vyote ambavyo anataka. Humuona kama shujaa wake, hivyo pale unapoahidi hakikisha kuwa ni kitu ambacho kiko ndani ya uwezo wako bila shaka yoyote. Epuka kumvunja moyo kwa jambo ambalo hutoweza kwa kuwa utavunja uaminifu wake kwako. Badala yake mwambie “nitajitahidi/nitajaribu”.

6. Wewe ni mjinga

Hili ni neno ambalo huwatoka kinywani wazazi wengi hasa wanapokuwa wamekwazwa na watoto wao. Lakini hili sio neno zuri kwa mtoto, litamjengea hali ya kushangaa kwa muda ila ukiendelea mara kwa mara atalizoea na ataona ujinga kama kitu cha kawaida. Kibaya zaidi anaweza kuanza kuwaita watoto wenzake jina hilo.

7. Usiogope /hakuna cha kuogopa

Watoto huwa na uoga kwenye masuala mengi sana. Kwa mfano mtoto mwingine huogopa paka, mbwa wa mapambo au hata kuku wa kufungwa. Unapomwambia usiogope mtoto huona kama unamdanganya wazi kwa kuwa anaona kuna kitu kinaogofya. Badala yake, mueleze kwa nini hatakiwi kuogopa hicho anachokiogopa ili umjengee ujasiri juu yake.

8. Na wewe Mlipizie/mrudishie

Ukiwa kama mzazi, mara kadhaa hujikuta unaumia kumsikia mwanao kaumizwa na mtoto mwenzake. Mara nyingi kwa makosa, mzazi hujikuta akimwambia mwanae alipize kisasi ili kumpooza mwanae na uchungu alioupata. Hilo ni kosa kubwa sana, kumfundisha mtoto kisasi kutamjengea moyo wa kulipiza visasi hata anapokuwa mkubwa. Badala yake msikilize na ulitatue tatizo hilo kwa kuwaonesha namna ambayo walistahili kufanya. Wakanye kwa haki na usawa bila kujali yupi ni mwanao.

9. Usinichoshe

Neno hilo ni fupi lakini ni baya sana kwa mtoto. Wazazi wengine hujikuta wakilitamka kwa mtoto hasa pale anaporudia mara kwa mara kitendo fulani au kuuliza sana maswali yaleyale. Unapomwambia hivi mtoto anaona kama unajutia uwepo wake na anaona kabisa haujali. Hii itamfanya aogope kukuuliza hata mambo mengine ya msingi akiogopa ‘utamshushua’. Hivyo hautakuwa sehemu ya kile anachokata kujifunza.

10. Funga domo lako

Kama lilivyo neno lenyewe halina ustaarfabu na limekaa kihasira na kikatili. Halifai kabisa kulitamka kwa mtoto. Kwa bahati mbaya wazazi wengine humwambia mtoto neno hilo pale anapolia. Kumbuka wakati huo mtoto huwa katika hisia za uchungu, unapomtamkia neno hilo anaweza kunyamaza lakini ataumeza uchungu wake na utakuja kuibuka tena hata ukubwani endapo utaendelea kuwa hivyo.

 

 

Mzee Wa Upako Anena Kuhusu Wanasisa Kuwafuata Viongozi Wa Dini
Dk. Slaa Akiri Kuwa Alipeleka Chadema Wazo La Kumchukua Lowassa Urais