Benchi la ufundi la klabu ya Parma ya Italia limemuamuru mshambuliaji kutoka Ivory Coast Gervais Yao Kouassi “Gervinho”, kufanya mazoezi ya pekee yake, kufuatia utovu wa nidhamu aliounyesha juma lililopita.

Gervinho aligoma kufanya mazoezi na wachezaji wenzake, kwa kushinikiza uhamisho wa kuondoka klabuni hapo, ili ajiunge na klabu ya Al-Sadd ya Qatari.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye aliwahi kutumikia Arsenal ya England kati ya mwaka 2011 hadi 2013, alihitaji kujiunga na Al-Sadd kupitia dirisha dogo la usajili, lakini dili la uhamisho hilo lilishindikana.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Parma imeeleza kuwa: “Baada ya kugomea mazoezi juma lililopita, Parma imemuamuru Gervinho kufanya mazoezi akiwa pekee yake, mpaka maamuzi mbadala ya benchi la ufundi yatakapotangazwa.”

Dili la mshambuliaji huyo lilishindwa kukamishwa dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili mwishoni mwa juma lililopita, na tayari vielelezo vya uhamisho wake vilikamilishwa kwa asimilia 50, lakini baadae mambo yalikwenda mrama.

Meneja wa klabu ya Al-Sadd Xavi alibnainisha wazi kuwa, Gervinho hatokua sehemu ya kikosi chake kwa msimu hu, na huenda wakajaribu kumsajili mwishoni mwa msimu.

“Kama tutamsajili itakua kwa ajili ya msimu ujao. Tunatambua ni mchezaji mzuri na anastahili kuwa nasi.” alisema kiungo huyo zamani wa Hispania na FC Barcelona.

Gervinho alijiunga na Parma mwaka 2018, akitokea Hebei China Fortune ya china aliyoifungia mabao 11.

Pia ana mkataba na klabu ya Parma hadi mwaka 2022, na kama angeondoka klabuni hapo uhamisho wake ungegharimu kiasi cha Euro milioni 5.5 sawa na Pauni milioni 4.6.

Gervinho ameshaifungia Parma mabao sita katika michezo ya michuano yote aliyocheza msimu huu, huku klabu yake ikishika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ya nchini Italia.

Spika achana hotuba ya Rais
Serikali yalifungia kanisa la Asembles of God Moshi