Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa ameliagiza jeshi la polisi  kuwakamata viongozi saba wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo mwenyekiti wao Freeman Mbowe kufuatia kifo cha mwanachuo Akwilina Akwiline kilichotokea pindi polisi walipokuwa wakituliza ghasia ya maandamano yaliyoanzishwa na kiongozi wa chama hicho.

Mbali na Mbowe viongozi wengine wanaopaswa kukamatwa ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu, John Mnyika na Salum Mwalimu.

Pia wamo, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema ( Bawacha), Halima Mdee, Mwenyekiti wa kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni muweka hazina wa Bawacha.

Kamanda wa Polisi Mambosasa amesema ” Hao ni watuhumiwa na kama wameitwa ni upendeleo tu, ila yaliyotokea wanapaswa kukamatwa”.

Hata huvyo Mkurugenzi wa itifaki na mawasiliano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema amesema ni kweli wamepokea barua hiyo ya wito wa jeshi la polisi ukiwata kuripoti ofisini kwao, ila kulingana na kuwa viongozi hao kuwa wametawanyika maeneo mbalimbali ya nchi katika kutekeleza majukumu ya nchi.

Hivyo ameliomba jeshi la polisi kuelewa mazingira hayo wakati taratibu nyingine zinafuata kutekeleza wito huo wa Jeshi la polisi  na kuepuka kuwa sehemu ya propaganda za kisiasa zinazoendelea, amedadafua Mrema.

 

 

TRA yatoa matokeo ya uchunguzi uliofanywa kwa Askofu Kakobe, na kubaini haya
Ndalichako akamata walimu wa chuo cha Kampala wasio na vibali