Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amesema uchunguzi juu ya kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT, Akwilina Akwiline bado unaendelea na mpaka sasa askari sita wapo chini ya ulinzi kusaidia kujua ni nani hasa alihusika na kifo hiko kilichotokea mapema mwanzoni mwa mwaka huu.

Mambosasa amesema hayo mapema leo hii pindi alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa pamoja na kuwashikilia askari hao bado haijafahamika moja kwa moja ni nani alihusika na mauaji hayo kwani hakuna ushaidi wa uhakika juu ya muhusika wa tukio hilo

“Wale walipokamatwa tulieleza bayana kwamba upelelezi unafanyika ili kujua ni nani ambaye ametenda kosa lile, bado suala la upelezi linaendelea’’

Amesema yapo maelezo yaliyotolewa ambayo bado yanafanyiwa kazi ili kubaini muhusika wa kifo hiko.

‘’Ikumbukwe silaha moja ambayo haijajulikana ni ipi ndio ilikwenda ikamgusa Akwilina, lakini kama ulivyojua askari walikuwa ni wengi lakini pia kulikuwa hakuna ushahidi kwamba yupi aliyekuwa ametenda hivyo, kwa hiyo uchunguzi bado unaendelea”, amesema Mambosasa.

Yapata mwezi sasa tangu mwanafunzi Akwiline, atutoke mnamo tarehe 17, Februari akiwa safarini kuelekea Bagamoyo ndipo mauti ilipomkuta akiwa ndani ya daladala na kupigwa risasi ya kichwa ambayo inaaminika kuwa ilitoka kwa mmoja wa askari aliyekuwa akijaribu kutuliaza ghasia za maandamano zilizoanzishwa na viongozi wa Chadema,

 

 

Bomberdier Q400 iliyokuwa imezuiliwa Canada kuwasili nchini
Waasi wavamia nyumba ya Rais Kabila