Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema suala la Dk. Shika kuingiza pesa zake Tanzania hana uhakika nalo na mtu kutumiwa hela kihalali si kosa ameongezea kuwa kama taarifa hizo ni za uongo anaweza kupuuzwa ila endapo kauli yake italeta madhara basi hatua zitachukuliwa.

Mambosasa amezungumza hayo leo pindi alipokuwa anaongea na waandishi wa habari akitoa ripoti za jeshi la polisi kuwashikilia watuhumiwa mbambali kwa kufanya makosa ya unyang’anyi kwa kutumia silaha za moto.

”Mtu kutumiwa hela kama ni halali aziingii kwenye pesa ambazo zinatakatishwa au hela ambazo zinapatikana kwa njia isiyo halali si kosa lakini kama ni muongo tu anajisema basi kuna mawili anaweza kupuuzwa lakini kama kauli zake zitamwaathiri yeyote anaweza kuja kulalamika na jeshi la polisi likachukua hatua” amesema Mambosasa.

Mambosasa amezungumza hayo pindi alipokuwa anajibu swali la mmoja wa waandishi wa habari baada ya kuhoji juu ya uhalali wa pesa za Dk. Luis Shika Kid ambaye hivi karibuni taarifa zimeeleza tayari ameingiza mabilioni yake ya fedha nchini Tanzania.

Aidha siku chache zilizopita Dkt. Louis Shika alivieleza baadhi ya vyombo vya habari nchini juu ya ujio wa fedha zake na baadhi ya vipande vya dhahabu zilizokuwa nje ya nchi kuwa tayari zimewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JKNIA) na kupelekwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa ajili ya kuhakikiwa.

Taarifa ambayo ilizua mjadala mkubwa mtandaoni ambapo watu wakionesha kutokuamini kwa ujio huo wa Dk. Shika wakidhani ni stori zisizo na ukweli ndani yake.

Hata hivyo Shika alithibitisha ujio wa mali hizo na kuonyesha baadhi ya nyaraka zinazothibitisha umiliki wa mali hizo.

Video: Itazame ngoma mpya ya Belle 9
Ajali mbaya ya basi yatokea nchini Uganda