Watuhumiwa Saba wa ujambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na Askari polisi katika eneo la Mwenge jijini Dar es salaam.

Kamanda wa polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa mbali na kuwaua watuhumiwa hao, polisi pia wamekamata bastora aina ya Bareta ikiwa na risasi tatu ndani ya kasha.

Amesema tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo ambapo watuhumiwa hao wakiwa ndani ya gari namba T956 BYA Toyota Noah, wanadaiwa walikuwa wakielekea kufanya uhalifu katika ghala la GS group l.t.d linalohifadhi vifaa vya pikipiki.

Mambosasa amesema walipata taarifa kutoka kwa msamalia mwema kuhusu njama za watu hao na kufika eneo la Mwenge Coca-Cola, na walipojaribu kulifuatilia gari hilo liliongeza mwendo na kuchepuka barabara ya vumbi ambapo walianza kulishambulia gari la polisi kwa risasi.

Amesema miili ya watu hao ipo hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa yeyote anayehisi nduguyake anaweza kuwa alihusika akaangalie na kumtambua.

Askari aliyemuokoa kichanga kwenye shimo la choo asimulia, aelezea maisha yake
Makonda ataka mkandarasi kukabidhi stendi ya Mbezi kwa wakati

Comments

comments