Askofu Gwajima mapema leo hii anatakiwa kuripoti kituo cha polisi kwa wito wa Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa kutoa maelezo juu ya video yake iliyosambaa mitandaoni akiwa faragha

Mambosasa amezungumza na Ayo TV na kusema kuwa Gwajima mapema leo hii Mei 8, 2019 anatakiwa kuripoti majira ya saa nne au saa tano katika  kituo cha polisi.

Ameongezea kuwa asipotokea atakamatwa kwani licha ya kuwa taarifa hizo hazijaripotiwa na mtu yeyote lakini wameziona mtandaoni.

Kamanda amesema kilichofanywa na Askofu Gwajima ni ukiukaji wa maadili.

”Tayari ameshaitwa aripoti, akichelewa atakamatwa, na tumemuita kwa sababu hakuna aliyelalamika lakini tumeona. Sisi tunachoendelea kusema ni vitendo vya ukiukaji wa maadili awe askofu awe mtu wa kawaida ila lililoonekana kwenye mitandao ni unyama ni kuuvua heshima ya utu wa mtu na kutundika kwenye karatasi”. amesema Mambosasa.

Aidha jana mitandaoni kumesambaa video iliyosemekana ni ya askofu Gwajima akiwa faragha huku akijichukua video.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 8, 2019
Mahakama yaamuru mali za DECI zitaifishwe

Comments

comments