Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa wamefanikiwa kumkamata Rajabu Muhamed maarufu kwa jina la Rajeshi mwenye umri wa miaka 25  ambaye anatuhumiwa kwa kuteka wamama, kuwabaka na kuwapora mali.

Mambosasa amesema kuwa mtu huyo hutumia gari aina ya Fun Cargo yenye namba T 172 BLH na kuwalazimisha wanawake kuingia kwenye gari hiyo na kuwatisha yeye ni Freemason na kuwataka  watoe mali zao, ikiwemo na paswedi ya kadi ya benki wasipofanya hivyo huwatishia kukata sehemu zao za siri.

Kamanda Mambosasa aliendelea kusema kuwa Rajabu Muhamed ameshawafanyia vitendo vya kinyama wanawake wengi sana hapa mjini ikiwa pamoja na kuwabaka na kuwadhalilisha.

“Anafanya vitendo vya unyang’anyi kwa kutumia nguvu hasa kwa wanawake, ubakaji na unyanyasaji wa kila aina, amefanya vitendo vingi sana mjini hapa vya unyanyasaji wa kina mama anawateka anajifanya ni Freemason anawapeleka mahali anapowapeleka na kuwafanyia vitendo vyote vya kinyama.

Ameongezea kuwa ”Huyu muhumi huyu anachoniambia mimi kwamba ameacha lakini amewadhuru wanawake wengi sana hapa mjini na wachache wenye ujasiri walifika kuripoti na ndiyo tukafuatilia na kufanikiwa kumtia mbaroni jana usiku maeneo ya Kinondoni”.

Aidha amesema kuwa Jeshi la polisi linawashikilia watu wawili wakike na wakiume waliohusika katika mauaji ya kiongozi wa Chadema kata ya Hananasif, Daniel John, majina ya watu hao yanahifadhiwa kwa sasa kwa sababu za kiupelelezi.

NEC yakamilisha uteuzi wa Diwani viti maalumu Chadema
Wanafunzi 111 wapotea baada ya shambulio la Boko Haramu