Kufuatia taarifa ya utekwaji wa mfanyabiashara Mo Dewji, Kamanda Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, Mkuu wa Mkoa Paul Makonda Pamoja na Maafisa polisi wakiongozwa na Naibu DCI wamefika eneo la tukio ambalo Mo Dewji ametekwa.

Kamanda Mambasasa amefunguka na kusema kuwa waliomteka ni wazungu wawili ambao bado hawajafahamika na dhumuni la utekeji bado halijajulikana ila jeshi la polisi limeanza ufuatiliaji wa tukio hilo.

”Niseme tu tukio hili limefanywa kwa kusimamiwa na wageni ambao ni wazungu wawili”.

Aidha Msemaji wa Simba, Haji Manara amewaomba wanasimba na wanachama wote wa Simba kutulia katika kipindi hiki ambapo vyombo vya usalama vikiwa vinafanya kazi yake, amesisitiza kuwa anaamini kuwa Mo atapatikana akiwa mzima.

”Niombe watu wote watulie, wanasimba watulie, wanachama watulie, wapenzi wote wa mpira watulie, familia yake imeniahidi kutulia, tukiacha vyombo kufanya kazi yake, tumeshake lakini tunaamini polisi wanavyombo vipana, kama kuna taarifa zaidi Kamanda ametoa namba zake tunaomba ushirikaono amemalizia Manara.

Mo Dewji ametekwa saa 11 alfajiri ya leo na watu wasiojulikana katika hoteli ya Colesseum anakofanyia mazoezi, ambapo watu hao walifyatua risasi juu na kuondoka nae.

 

 

Video: Mwendokasi vurugu tupu, Majaliwa, Dk Bashiru wahofia kura za JPM
Mbunge mwingine wa Chadema ajiuzulu

Comments

comments