Mbunge wa Kibamba, Issa Mtemvu na mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori wameongoza mamia ya waombolezaji katika ibada ya mazishi ya familia ya ndugu watano wanaodaiwa kufariki kwa kukanyagwa katika shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza katika maombolezo hayo, Mtemvu amesema kuwa kazi ya Mungu haina makosa na kila kifo kina sababu zake ambapo ametoa salamu za rambirambi kwa familia.

“Nitoe pole kwa familia hatuwezi kulaumu kwa sababu hili ni jambo la bahati mbaya. Kila kifo kinatokea kwa sababu na ndio maana kuna mwingine ataumwa kichwa. Kazi ya Mungu haina makosa,” amesema Mtemvu

Ndugu hao wa familia ya Daudi Mtuwa ni  Susan Mtuwa na watoto wake wawili Nathan (6) na Natalia (5) pamoja na watoto wengine wawili Cris (11) na Michelle (8) wa shemeji zake Susan walifariki dunia katika shughuli hiyo iliyofanyika Jumapili Machi 21, 2021.

Watoto hao wanatarajia kuzikwa leo saa 10 jioni eneo la nyumbani kwa Mtuwa, Kimara mkoani Dar es Salaam.

Waitara: Magufuli alikuwa na dhamana kiutendaji
Didier Gomes aitambia AS Vita