Polisi nchini Belarus wamewakamata watu 633 katika maandamano yaliyofanyika nchi nzima jana Jumapili.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani imeeleza   kuwa maafisa walianzisha hatua ya kuwafuatilia waandamanaji wanaompinga rais Alexender Lukashenko .

Wakati huohuo, taarifa kutoka ikulu ya Urusi leo imeeleza kwamba kiongozi huyo wa Belarus atakwenda nchini Urusi siku chache zijazo kwa ajili ya mazungumzo na serikali, mjini Moscow.

Maandamano hayo yasiyo ya kawaida yalizuka baada ya Lukashenko aliyeitawala Belarus kwa miaka 26, kudai kuwa amechaguliwa tena kwa asilimia 80 katika uchaguzi uliofanyika Agosti 9.

Mbeya City yaweka rekodi Dar es salaam
MCT yaeleza sababu kucheleweshwa tuzo za EJAT