Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo ya kunyesha kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini kuanzia leo Alhamisi na kesho Ijumaa.

Taarifa ya TMA imebainisha mikoa itakayokumbwa na mvua hizo ni Pwani ya Kusini ambayo ni Lindi na Mtwara, Nyanda za Juu Kusini Magharibi ambayo ni Mbeya, Iringa, Songwe na Rukwa, Dar es Salaam na Pwani.

“Upepo wa Pwani, unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini; kwa kasi ya Km 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza;

“Hali ya Bahari, inatarajiwa kuwa mawimbi madogo hadi makubwa kiasi na matazamio kwa siku ya Ijumaa Januari 5,2018, kuongezeka kwa mvua katika mwambao wa Pwani na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi.”

Hata hivyo, tayari mvua hizo zimekwisha kuanza na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani mvua ilinyesha jana Jumatano usiku katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo.

Mapacha walioungana wafanyiwa uchunguzi zaidi wa kiafya
Jukata kufungua kesi dhidi ya katazo la maandamano