Hatimae klabu Manchester City imetajwa kuwa katika mikakati ya kutaka kumsajili beki kutoka nchini Ufaransa, Aymeric Laporte kama walivyoelekezwa na meneja wao mtarajiwa Pep Guardiola.

Taarifa kutoka nchini Hispania zinaeleza kwamba, uongozi wa klabu ya Athletic Bilbao inayomiliki beki huyo, umewataka Man city kujipanga vilivyo katika jambo hilo na kama watakwenda na ofa iliyo chini ya paund milion 40, hawatopewa ruhusa ya kufanya mazungumzo.

Laporte, mwenye umri wa miaka 21, naye ameripotiwa kuwa tayari kuelekea nchini England kutokana na hitaji lake la kutaka kubadilisha mazingira ya  soka ambalo amekua akicheza huko nchini Hispania tangu mwaka 2010.

Man City wametajwa kuwa tayari kumsainisha beki huyo mkataba wa miaka mitano.

Hendrik Johannes Cruijff Afariki Dunia
Chelsea Wambembeleza Baba Yake Mats Hummels