Klabu ya Man City imethibitisha kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Brazil Gabriel Fernando de Jesus kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 27 akitokea Palmeiras.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19, amekamilisha usajili huo kwa masharti ya kujiunga na Man City itakapofika mwezi januari mwaka 2017 na amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano ambao utafikia kikomo 2021.

“Manchester City ni moja ya klabu bora duniani, na nimefarikjika kujiunga nayo,”

“Ninatarajia mambo makubwa nitakapokua hapa kutokana na uwepo wa wachezaji wenye uwezo, naamini nitajifunza mambo mengi kutoka kwao.” Jesus aliiambia Tovuti na klabu hiyo ya Etihad Stadium.

Jesus alifunga mabao 26 katika michezo 67 aliyocheza akiwa na Palmeiras, na anatarajia kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoiwakilisha Brazil kwenye michezo ya Olimpiki.

Jesus anakua mchezaji wa sita kusajiliwa na Man City katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, baada ya kutanguliwa na Leroy Sane, Ilkay Gundogan, Nolito, Oleksandr Zinchenko na Aaron Mooy.

VfL Wolfsburg Wakata Ngebe Za Julian Draxler
Roberto Martinez Aula, Akabidhiwa Jahazi La Ubelgiji