Klabu ya Manchester City, imethibitisha kumsajili kiungo Anthony Caceres ambaye alikua akiitumikia klabu ya Central Coast Mariners ya pwani ya kusini mashariki mwa Australia.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, atajiunga na klabu ya Man city wakati wowote ndani ya mwezi huu, ili kukamilisha mipango ya meneja Manuel Pellegrini ambaye bado anaamini kikosi chake kina nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa nchini England msimu huu.

Hata hivyo usajili wa Caceres, umewashtua wengi kutokana na mchezaji huyo kutofahamika vyema na hata klabu iliyokubali kumuachia haijulikana vyema ulimwenguni kote.

Caceres anaondoka Central Coast Mariners, huku akiacha kumbukumbu ya kucheza michezo 62, katika ligi ya New South Wales (A-League) na amefanikiwa kufunga mabao matatu tangu aliposajiliwa mwaka 2012 akitokea Marconi Stallions.

“Hatuna budi kufurahia hatua kubwa ambayo imefikiwa na Caceres, imetupa heshima sisi watu wa klabu ya Central Coast Mariners, kwa kusajiliwa na klabu kubwa duniani. Inaonyesha tupo vizuri na tuna uwezo wa kuwaendeleza wachezaji ambao wana uwezo wa kucheza popote pale dunaini,” amesema meneja wa klabu hiyo Tony Walmsley.

“Wakati nilipo msajili Anthony Caceres, nilijua kuna siku atafanikiwa kusonga mbele, na leo hii kila mmoja wetu ameona suala hilo likifanikishwa na Man city.

Hii inakua ni mara ya kwanza kwa Man city, kufanya usajili wa mchezaji kutoka kwenye nchi ya New South Wales.

Radamel Falcao Asaka Mbinu Za Kujinusuru
Magwiji Wa Tennis Kuanza Na Vibonde Australian open 2016