Hatimaye Klabu ya Manchester City imemaliza minong’ono kwa kumsajili rasmi mshabuliaji Raheem Sterling.

Kinda huyo amekamilisha uhamisho wake wa Paund Milioni 49 kutoka Liverpool baada ya kufaulu vipimo vya afya na kocha Manuel Pellegrini amesema kumsajili Sterling kuna-maanisha amepata moja ya wachezaji wazuri wa ushambuliaji katika dunia ya soka.

Kocha huyo kutoka nchini Chile amesema Sterling ni mmoja kati ya wachezaji wazuri katika nafasi ya ushambuliaji katika dunia ya soka, na ameahidi kumjumuisha katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi ambapo Man City wataelekea nchini Australia baadae juma hili.

Klabu hizo mbili Jumapili zilifikia makubaliano ya biashara ya nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza na sasa anakaribia kusaini kikosi cha Manuel Pellegrini.

City iligonga mwamba katika ofa zake mbili za awali juu ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye amepigwa picha akitoka kwenye hospitali ya Manchester kabla ya kufikia makubaliano mwishoni mwa wiki.

Sterling hakwenda na kikosi cha Brendan Rodgers katika ziara ya kujiandaa na msimu barani Asia ili kushughulikia uhamisho wake Etihad.

City wamewalipa wapinzano wao hao katika Ligi Kuu ya Uingereza Pauni Milioni 49, wakati Sterling atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 180,000 kwa wiki.

Huo ni uhamisho wa saba wa bei kubwa zaidi kuhusisha klabu za Uingereza.

Sterling, ambaye Mkataba wake Liverpool ulikuwa unamalizika mwaka 2017, atakuwa mchezaji ghali zaidi wa Uingereza kihistoria.

Tathmini za karibuni zilimuweka mchezaji huyo katika thamani ya mchezaji ghali zaidi mdogo katika soka ya Ulaya, akifuatiwa na beki wa Paris Saint-Germain, Marquinhos na mchezaji mpya wa Manchester United, winga Memphis Depay.

Yanga Wamalizana na KMKM, Wamchukua kihalali Mudathir Khamis
Huddah adai alikuwa ‘Kayai’ wa Mzee Ojwang!