Timu ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Real Salt Lake katika mchezo wa kirafiki uliofanyika huko nchini Marekani.

Real Salt Lake ndio walio kuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Luis Silva dakika ya 24  kabla ya Henrik Mkhitaryan kusawazisha katka dakika ya 29.

Manchester United walionekana kucheza vizuri sana na mnamo dakika ya 38 mshambuliaji mpya Romelu Lukaku aliifungia Man Utd bao la pili baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Mkhitaryan.

Lukaku aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 75 ameanza kuonyesha thamani yake baada ya kucheza kwa kiwango cha juu katika mchezo huo na kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza akiwa Man Utd.

Huu ni mchezo wa pili kwa Man Utd kupata ushindi huko Marekani ambapo timu hiyo imeweka kambi baada ya mchezo wa kwanza kushinda dhidi ya La Galaxy kwa ushindi wa 5-2.

Katika mchezo huo beki wa wa kulia Antonio Valencia wa Man Utd alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa timu ya Real Salt Lake Sebastian Saucedo katika dakika ya 68.

 

 

Lowassa kuburuzwa kortini
Trump aionya Venezuela, aitaka kutobadili Katiba ya nchi hiyo

Comments

comments