Licha ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Manchester United imetajwa kuwa klabu yenye thamani kubwa katika vilabu vyote vya soka barani Ulaya.

Klabu hiyo imetajwa kuwa na thamani ya £1,357m pesa hizi zikitokana na namna ambavyo mechi zao zinarushwa na kiasi cha pesa ambacho timu zote za EPL hupewa.

Hapa chini ni orodha ya vilabu 10 vyenye dhamani kubwa barani Ulaya;

  1. Manchester United (£1,357m)
  2. Real Madrid (£1,127m)
  3. FC Barcelona (£1,082m)
  4. Bayern Munich (£1,007m)
  5. Manchester City (£953m)
  6. Liverpool (£862m)
  7. Chelsea (£856m)
  8. Arsenal (£776m)
  9. PSG (£654m)
  10. Tottenham (£548m)

Utafiti unaonyesha kuwa Man Utd inathamani ya paundi milioni 1,357 ikiwa ni paundi milioni 404 zaidi ya Manchester City ambayo ni klabu ya pili kwa thamani katika vilabu vya Uingereza.

Fisi 12 wauawa 1 akutwa na shanga kiunoni
Faiza Ally atamani kukutana na mmiliki wa Instagram 

Comments

comments