Mashetani wekundu wa Old Trafford, Manchester Utd na klabu ya washika bunduki ya Arsenal, leo wameshindwa kumpata mbabe baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi ya ligi Kuu ya Uingereza.

Manchester walikuwa wa kwanza kuzichoma nyavu za Arsenal dakika ya 69 baada ya Juan Mata kufanya kweli akipokea mpira ulioanzaishwa kutoka kulia na Pogba ukipitia kwa Herrera.

goli-1

Hata hivyo, furaha za Manchester zilizimwa ghafla katika dakika ya 89 baada ya Oliver Giroud kufumania nyavu kwa kichwa akipokea mpira uliochongwa na Alex Oxlade-Chamberlain.

goli

Matokeo hayo yaliyowagawia pointi 1 kila mmoja yanaiweka Man Utd katika nafasi ya 6 akiwa na pointi 19 huku Arsenal wakikaa nafasi ya 3 kwa pointi 25.

Mzee Wenger ataukumbuka uamuzi wake wa busara wa kumuingiza Giroud dakika ya 73 akichukua nafasi ya Elneny.

Kocha Jose Mourinho ameendelea kuweka rekodi nzuri ya kutofungwa na Arsenal katika Ligi Kuu, ameshinda mara tano na kutoa sare mara 12.

#HapoKale
Madiwani watakiwa kupima ardhi haraka, kujiandaa na uwekezaji