Pale nchini England stori inayozidi kuongelewa kwenye maduka mbalimbali ya kuuzia chakula na vinywaji ni usajili wa winga wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England, Jadon Sancho.

Sancho anatajwa sana kwamba atajiunga na Man United katika dirisha hili baada ya dili lake kushindikana kwenye dakika za mwisho mwanzoni mwa msimu huu 2020/21.

Baada ya kikao cha mabosi wa Man United imeripotiwa wanatarajia kuwasilisha ofa mpya itakayokaribia Pauni 86 milioni ambayo Dortmund ndio inaihitaji kwa sasa ili kumuuza Sancho.

Taarifa zinafafanua kwamba dili hilo limebakia kwa Dortmund pekee kwani, wawakilishi wa Man United wameshamalizana na wawakilishi wa Sancho katika maafikiano ya masilahi binafsi ya mchezaji na dili litakuwa ni la miaka mitano kwa sababu hadi masuala ya mishahara wameshakubaliana.

Man Utd wanatarajia kupata zaidi ya Pauni milioni 100, endapo watafanikwa kumuuza kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba, ambaye anawaniwa na PSG mjini Paris.

Mashetani Wekundu wanatarajiwa kutumia fedha watakazozipata kwenye usajili wa kiungo huyo, kufanya maboresho ya kikosi chao katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya England, ambao utaanza mapema mwezi Agosti.

Jokate awashukuru Kisarawe, aahidi Temeke mpya
UEFA EURO 2020: Bingwa mtetezi mtegoni