Rais wa klabu ya Benfica Luis Filipe Vieira ameripotiwa kutua mjini Manchester kwa ajili ya kumalizana na uongozi wa klabu ya Man Utd, kuhusu dili la kiungo Renato Júnior Luz Sanches.

Man Utd wameonyesha nia ya dhati ya kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18, na wamedhamiria kumaliza dili la usajili wake kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili mwishoni mwa msimu huu.

Vieira, ameonekana akiwa na baadhi ya maafisa wa Man Utd na baadhi ya vyombo vya habari vimeanza kuhusisha ujio wake la suala la usajili wa Renato ambaye anaripotiwa kuwa na kipaji cha kusakata kabumbu cha hali ya juu.

Mbali na uwepo wa rais wa klabu ya Benfica, pia wakala wa Renato naye anatajwa kuwepo mjini Manchester na mapema hii leo alionekana katika moja ya hoteli kubwa za mjini humo.

O Jogo spread claims the Benfica president is in Manchester to discuss Renato SanchesSehemu ya gazeti inayothibitisha uwepo wa rais wa klabu ya Benfica huko mjini Manchester nchini England

Renato yupo chini ya wakala Jorge Mendes, ambaye amekua na mahusiano mazuri na uongozi wa Man utd linapojitokeza suala la wachezaji wake kuhitajika huko Old Trafford.

Thamani ya Renato itajwa kufikia kiasi cha Pauni million 40 na Man Utd wameonyesha kutokua tayari kulipa kiasi hicho cha pesa kwa kutaka kufanya mazungumzo mapya ili kutoa nafasi ya mmoja wa wachezaji wao kuhusika na uhamisho wa kiungo huyo.

Hata hivyo haijafahamika ni mchezaji gani ambaye atapewa nafasi ya kuwa sehemu ya kusajiliwa na Renato ili aelekee Benfica kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ya huko nchini Ureno.

Katika hatua nyingine meneja kutoka nchini Ureno, Jose Mourinho ambaye anahusishwa na mipango ya kupewa ajira huko Old Trafford, kama mbadala wa Louis van Gaal anatajwa kuwa shabiki mkubwa wa Renato Sanches.

Siku kadhaa zilizopita Mourinho alikua anahusishwa na mipango ya kutaka kuona Renato anasajiliwa klabuni hapo, kutokana na kuamini ujio wake huenda ukaleta mapinduzi ya kiushindani kwenye kikosi cha mashetani wekundu.

Renato alikuzwa na kuendelezwa na klabu ya Águias da Musgueira kuanzia mwaka 2005–2006 na baadae alisajiliwana Benfica na kuingizwa katika kikosi cha vijana ambacho alikitumikia kuanzia mwaka 2006 hadi 2014 na kisha alipandishwa katika kikosi cha kwanza.

MTANDAO WA WIZARA KENYA WAVAMIWA
Gonzalo Gerardo Higuaín Awekwa Sokoni Rasmi