Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, hii leo linatarajia kupanga ratiba ya michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya mtoano baada ya mapambano wa hatua iliyopita kukamilishwa usiku wa kuamkia jana.

Maafisa wa UEFA kwa kushirikiana na maafisa wa klabu zilizoingia kwenye mchakato wa kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo msimu wa 2015-16, Watakutna mjini Nyon nchini Usiwz kukamilisha zoezi hilo.

Klabu 20 zitahusishwa katika mchakato huo ambao utakamilishwa kwa michezo 10 tofauti itakayotoa majibu ya kupatikana kwa klabu 10 zitakazotinga kwenye hatua ya makundi.

Hafla ya upangaji wa ratiba ya michezo hiyo ya mtoano, inatarajia kufanyika mishale ya saa sita mchana kwa saa za nchini Uswiz.

Timu zilizosonga mbele kupitia michezo ya mtoano iliyochezwa tangu mwezi Juni ni;

FC Basel 1893 (SUI) 84.875

Celtic FC (SCO) 39.080

APOEL FC (CYP) 35.460

FC BATE Borisov (BLR) 35.150

GNK Dinamo Zagreb (CRO) 24.700

Maccabi Tel-Aviv FC (ISR) 18.200

FK Partizan (SRB) 14.775

Malmö FF (SWE) 12.545

KF Skënderbeu (ALB) 5.575

FC Astana (KAZ) 3.825

 

Timu zilizoingia katika hatua ya mtoani kwa kutumia vigezo vya kumaliza kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi ya nchi husika ni;

Manchester United FC (ENG) 103.078

Valencia CF (ESP) 99.999

Bayer 04 Leverkusen (GER) 87.883

FC Shakhtar Donetsk (UKR) 86.033

Sporting Clube de Portugal (POR) 56.276

PFC CSKA Moskva (RUS) 55.599

SS Lazio (ITA) 49.102

Club Brugge KV (BEL) 41.440

AS Monaco FC (FRA) 31.483

SK Rapid Wien (AUT) 15.635

Thierry Henry: Arsenal Bingwa 2015-16
Siku Moja Baada Ya Kuzaliwa, Mtoto Wa Diamond Apata Ubalozi