Taarifa za ndani kutoka SSC Napoli zinadai Klabu ya Manchester United imeshafanya makubaliano na mabosi wa klabu hiyo juu ya uwezekano wa kumsajili beki kisiki Kim Minjae mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Beki huyu wa kimataifa wa Korea Kusini alikuwa sehemu ya ukuta mgumu ulioiwezesha  SSC Napoli kutwaa taji la Ligi Kuu ya Italia, Serie A msimu huu 2022/23, huku mkataba wake ukitarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Man United ambayo imekuwa na upungufu kwenye eneo lao la ulinzii msimu huu kutokana na majeraha ya mara kwa mara ambayo yaliwakumba mabeki wake, inaamini ujio wa Kim utaongeza ufanisi kwa kuwa haitakuwa na presha pale Raphael Varane ama Lisandro Marfinez mmoja wao akiumia.

Inadaiwa makubaliano baina ya mchezaji huyo na Man United yalishafanyika muda mrefu na kilichokuwa kimebakia ni United kukubaliana na Napoli ambapo sasa makubaliana yao yamefikia asilimia 70.

Man United jana Alhamis (Mei 25) iliivaa Chelsea katika kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hassan Dilunga kuvaa gwanda Msimbazi 2023/24
Saba wa familia moja wafariki kwa kufukiwa na tope