Klabu ya Man Utd, hatimae imekubali ada ya usajili wa kiungo kutoka nchini Ufaransa, Paul Pogba baada ya ofa yao ya Pauni milioni 85 kuwekwa kapuni na mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus.

Gazeti la L’Equipe la nchini Ufaransa, limeripoti kuwa Man Utd wamekubali kutoa kiasi cha Euro milioni 120 kwa ajili ya kukamilisha mpango wa kumrejesha Pogba, Old Trafford baada ya kukubali kumuachia mwaka 2012.

Kutokana na taarifa hizo, kuna uwezekano kwa viongozi wa Juventus wakakubali kukaa chini na Man Utd kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya usajili wa Pogba, ambaye tayari inaonesha ataondoka mjini Turin katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Meneja wa Man Utd, Jose Mourinho amekua mstari wa mbele kuhakikisha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 anasajiliwa klabuni hapo, kutokana na mikakati aliyojiwekea ya kufanya vyema msimu wa 2016/17 ambao umepangwa kuanza mwezi ujao.

Panga lingine lafyeka mishahara wafanyakazi NSSF
Mrema kuwaombea msahama kwa Magufuli wafungwa wa Dawa za kulevya, Ujambazi kwa sharti hili