Majogoo wa jiji Liverpool, wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA Europa League, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Manchester United usiku wa kuamkia hii leo.

Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Anfield, bao la kwanza la Liverpool lilifungwa na Daniel Sturridge kwa penati dakika ya 20, baada ya Nathaniel Clyne kuangushwa na Memphis Depay kwenye eneo la hatari.

Mshambuliaji Mbrazil, Roberto Firmino Barbosa de Oliveira, akaongeza matumaini kwa Liverpool kwenda hatua ya robo fainali baada ya kufunga bao la pili dakika ya 73

Man Utd watatakiwa kushinda 3-0 katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora utakaochezwa machi 17 kwenye uwanja wa Old Trafford, ili kujihakikishia nafasi ya kutinga katika hatua ya robo fainali.

Matokeo ya michezo mingine ya mkondo wa kwanza ya UEFA Europa League, hatua ya 16 bora iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Sparta Prague 1-1 Lazio

Athletic Club 1-0 Valencia CF

Villarreal 2-0 Bayer 04 Leverkusen

FC Basel 0-0 Sevilla

Borussia Dortmund 3-0 Tottenham Hotspur

Fenerbahce 1-0 Sporting Braga

Shakhtar Donetsk 3-1 RSC Anderlecht

Herve Renard Ataja Kikosi Cha Morocco
Aliyedai Rais Mugabe ni Mzee aburuzwa mahakamani