Mtayarishaji wa ‘hit song’ ya Ali Kiba ‘Seduce me’, Man Walter amesema wimbo huo umerekodiwa miaka miwili iliyopita na haukuwa kwenye mipango ya kuachiwa hivi karibuni.

Walter amesema ‘Mfalme Kiba’ ana nyimbo nyingi studio ambazo hazijatoka na kwamba tayari kuna wimbo mwingine ambao walikuwa wamepanga kuutoa tofauti na ‘Seduce Me’ kumaliza kiu ya mashabiki waliokuwa wanahitaji sana wimbo mpya.

Akifunguka kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio, Walter amesema waliamua kuutoa wimbo huo kwa uharaka kwani wimbo waliokuwa wamepanga kuutoa ulikuwa bado haujakamilika.

“Seduce me ilirekodiwa miaka miwili iliyopita. Ali aliponiambia anataka kutoa wimbo sasa hivi ndiyo ikabidi tuitafute tena tusikilize upya na mwisho tukaanza kurekebisha baadhi ya sehemu,” alifunguka.

“Na katika akiba ya Ali huu ndio wimbo wa kistarabu, kuna ngoma nyingine kali sana tulitoa huu kwakuwa attention (umakini) ya watu ilikuwa kubwa sana,” aliongeza.

Man Water amekuwa akitayarisha nyimbo nyingi za Ali Kiba ukiwemo wimbo ulio mrudisha kwenye game ‘Mwana” miaka michache iliyopita baada ya kuaka kimya kwa muda mrefu.

Video: Ofisi za IMMMA zililipuliwa na milipuko wa kienyeji- Polisi Dar
Watuhumiwa wa kula nyama za binadamu wakosa dhamana