Mtayarishaji mahiri wa muziki hapa Bongo na mmiliki wa studio za Combination sound, Man Walter amefunguka kuhusu kauli ya Alikiba aliyosema kuwa rasmi ameacha kufanya nae kazi kwa sababu alizotaja kuwa amekuwa akichelewesha sana kutoa kazi lakini pia amekuwa msumbufu.

Katika moja ya chombo cha habari hapa nchini Alikiba alisikika akisema.

”Man walter hadi akupe kazi uwe umefanya kazi, ni msumbufu sana amekuwa na sababu nyingi, anachelewesha sana kazi na anafanya anapojisikia” amesema Alikiba.

Akijibu tuhuma hizo Man Walter amesema kuwa kitu kinachompelekea asitoe baadhi ya kazi za Alikiba ni kwamba kuna baadhi ya ngoma amekuwa akimdai hajazilipia huku ngoma nyingine akiwa amezitoa kwa kutumia watayarishaji wengine.

Ambapo ametaja ngoma nne ambazo anazidai na tayari zimeachiwa bila kulipiwa na kila ngoma inagharimu pesa taslimu milioni moja, ngoma hizo ni Mbio, Mshumaa, Mwambie sina na ngoma moja ambayo bado haijaachiwa rasmi aliyoipa jina la Kupedikalee.

”Milioni moja mi kwangu kubwa sana, na ndio maana naipambania kwahiyo akisema mi sishindwi pesa ndogo nafikiri anaabuse kipato ambacho mimi nashiriki na familia yangu”

Hata hivyo Alikiba amesema kuwa kiasi cha pesa anachodaiwa na Man Walter ni kiasi kikubwa sana ambapo hata akiamua kukilipa anaweza ila hajakilipa kutokana kwamba aliamua kususa nyimbo zake zote ambazo zipo kwa Man Walter.

Aidha Man Walter ameipongeza sana menejiment ya Alikiba iliyopita kwa jitihada kubwa ambazo walikuwa wanafanya kumsukuma Ali kufanya kazi amesema sasa anasubiri kuona utendaji kazi wa menejimenti mpya ya Alikiba.

”Naipongeza menejiment ya Ali chini ya Seven, nimesikia kwamba haipo tena lakini ilikuwa inafanya kazi very proffesional, sasa tuone itaendaje bila ile menejimenti ya mwanzo, na huenda seven angenilalamikia kwanini sijamletea huenda angekuwa ameshanilipa kwani ngoma zote tulizofanya chini ya Seveni zimeshalipiwa kama vile Seduce me, Mvumo wa radi, sidai kabisa”. Ame

Aidha ameshauri watu wajue namna ya kuchukuliana, kupishana kunatokea.

 

Ukame Australia: Maelfu ya Ngamia kuuawa
Waziri Kabudi afafanua mchango wa UNICEF nchini

Comments

comments