Aliyekuwa Mkuu wa Idara Habari ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Haji Manara, amefunguka kuhusu tukio la Muwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji ‘Mo’ kukabidhi Shilingi Bilioni 20 kwa bodi ya wadhamini ya klabu hiyo.

‘Mo’ alikabidhi fedha hizo kama alivyoahidi wakati wa mchakato wa mabadiliko ndani ya Simba SC, katika hafla fupi iliyofanyika jana Ijumaa (Julai 30) jijini Dar es salaam.

Manara ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kufunguka juu ya hatua hiyo iliyoshuhudiwa na waandishi wa habari.

Manara ameandika: Nikisoma baadhi ya Comments zenu toka jana mnauliza Bughatti Mbona husemi kitu kuhusu billioni 20?

Ndugu zangu kama kuna Muumini namba moja aliyeshiriki kuwashawishi Wanasimba wakubali juu ya muundo huu mpya ni mm, nilizodolewa sana, nikatusiwa sana na nikagombana na wengi kuhusu uwekezaji huu, iweje nisiunge mkono jambo lenye maslahi kwa Simba na mpira wetu Kwa ujumla?

Na niwaambie jana ni siku kubwa kwangu Kwa sababu nililotaka na kulipigania limekuwa.

Ninawezaje kupinga uwekezaji wakati ni mm niliyekuja kwenu ktk Mkutano mkuu kuwaomba Wanachama hata jina la uwanja liitwe Kwa jina Simba MO Arena na mkanikubalia?

Ninyongeni muwezavyo lakini legacy yangu msiidharau.

Nitaunga mkono kila jitihada za kuifanya Simba iwe kubwa zaidi na zaidi na Insha’Allah wiki hii ntaongea nanyi kuwashukuru.

Mm ni binadaam nisiyekamilika kama tulivyo wote wengine, so lazma nije kusema sorry pale nilipoteleza na Insha’Allah Mungu ataendelea kutusimamia Kwa kila hatua.

Nawapenda na ntawapenda always Wanasimba na Watanzania.

Simba Nguvu Moja

Serikali ya Zanzibar yaapa kuulinda Muungano
Usajili wa wakulima washika kasi