Afisa habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa kukaa juu ya msimamo wa ligi kuna raha yake lakini haitakuwa na maana endapo watapoteza au kutoka sare kwenye mchezo wa leo dhidi ya timu ya Maji Maji.

Amesema kuwa Maji Maji ni timu nzuri na wanaiheshimu kwa historia yake kwenye soka la Tanzania pamoja na rekodi yao nzuri ilipokutana na timu zinazofanya vizuri msimu huu.

“Maji Maji ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri na rekodi zao ni nzuri kwa timu ambazo zinafanya vizuri msimu huu Yanga, Singida United, Azam na hata Prisons hakuna timu iliyowafunga Maji Maji kwa hiyo sisi hatuendi pale tukiwa tunawadharau, tunajua tunahitaji pointi tatu.”amesema Manara

Aidha, amesema kuwa wachezaji wa Klabu hiyo wameahidi kujituma na kuhakikisha wanapata pointi tatu ili kuendelea kukaa kileleni kwa uhuru zaidi.

Hata hivyo, kuhusu presha ya Azam na Yanga ambazo zipo nyuma yao, Manara amesema timu hizo haziwashughulishi wanachoangalia ni timu wanayokutana nayo.

Habari picha: JPM ashiriki Ibada katika Kanisa la Mtakatifu Petro Jijini Dar
Conte adai anafuraha kuendelea kuinoa Chelsea