Hatimae uongozi wa Klabu ya Simba SC umetoa sababu kwa nini hawakuweka wazi kosa alilofanya kiungo Jonas Mkude hadi kufikia hatua ya kusimamishwa kwa muda, kabla ya kuomba radhi jana Alhamis (Januari 21), kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Simba wamejibu suala hilo ambalo kwa kipindi cha majuma mawili lilikua gumzo, huku uongozi wa klabu hiyo ukishinikizwa kusema kosa la Mkude.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Ramadhan Manara amesema kutoliweka wazi kosa alilofanya kiungo huyo ni utaratibu waliojiwekea ndani ya klabu, na wanaamini kufanya hivyo ni kulinda heshima na utu wa aliefanya kosa.

“Binaadamu wote makazini kwetu wakati mwingine tunakosea, ni Very Unprofessional tukianza kuanikana makosa yetu hata sisi wenyewe maofisini kwetu,”

“Yaani kuna ule utu, unaweka utu mbele kuliko stori yenyewe, jichukulie wewe uliharibu, halafu bosi ama ofisi yako iamue kutangaza madhambi yako kwenye Public, au kumwambia hata mkeo au mume wako, utajifikiria vipi?”

“Simba ni klabu kubwa, ina utaratibu wake wa kutoa habari, itoshe kusema kwamba alifanya makosa ya kinidhamu na alisimamishwa, jambo lake lipo kwenye kamati ya Maadili, nadhani kesho kama alivyosema CEO watalimazika, na bado ya hapo New Page itafunguliwa.” Amesema Manara.

Balozi Ibuge akutana, kufanya Mazungumzo na AG Zanzibar
IGP Sirro ajitambulisha rasmi