Mkuu wa Idara yaHabari na Mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Manara ameonesha kukasirishwa na kitendo cha Mshauri wa Uongozi wa Young Africans Senzo Mazingiza Mbatha kukutana na kocha Mkuu wa Al Ahly Pitso Mosimane usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es salaam.

Manara ameonesha kukasirishwa huko kwa kuandika maneno mazito kupitia kurasa zake za mitanbdao ya kijamii, akimtuhumu Senzo ambaye aliwahi kuwa Afisa mtendaji mkuu wa Simba SC, kabla ya kuahamia Young Africans mwaka 2020.

Katika maneno yaliyoandikwa na Manara ni dhahir inaonesha anaamini Senzo alikutana na Pitso, kwa lengo la kuihujumu Simba SC, ambayo leo jioni itashuka dimbani kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wamzunguuko wa pili wa ‘KUNDI A’.

Manara ameandika: “Wananchi hamna ubingwa mwaka wa tatu, wananchi wanataka kujitoa katika ligi. Nani kawaambia Yanga wana haki kuliko wengine. Senzo nilikuwa namheshimu sana, alipoondoka nilituhumiwa sana, nikasema yes ni rafiki yangu na ninampenda. Lakini katika vitu amefanya ni jana, ni mambo ya hovyo kabisa,”

“Wewe una tuhuma za kuhujumu Simba (Senzo), Simba imetuhumu na kesi iko polisi. Eti watu wanasema eti wanafahamiana, wote ni raia wa Afrika Kusini. Sawa, swali langu angekuwa ni CEO wa Simba, angekwenda kumsalimia Pitso usiku wa kuamkia mechi, angefanya hivyo,”

Julio ajitetea kutolewa AFCON U20
Sauko: Simba SC msitembee na matokeo mkononi