Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa afisa habari wake, Haji Manara, umesema kuwa malengo yao msimu huu ni kufikisha alama 100 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Manara amesea hayo kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa jana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Manara ameeleza kuwa wanatamani kufikisha alama hizo ili kuweka rekodi ya aina yake japo amekiri si rahisi sababu kila timu ina malengo ya kupata matokeo.
“Msimu huu tuna malengo ya kufikisha alama 100 kwenye ligi ili kuweka rekodi ya aina yake.
“Najua ligi ni ngumu na kila timu inapanga kushinda hivyo lazima tukutane na changamoto, Simba haiwezi kushinda kila kitu,”alisema Manara.
Hawa ndiyo viongozi wanaoapishwa na Rais Magufuli leo
Zahera ageukia madai ya ushirikina Yanga