Msemaji wa klabu ya Young Africans Haji Manara ameibuka na jambo jipya katika mitandao ya kijamii, kwa kuweka andiko lililobeba dhana yenye fumbo la usajili.

Manara ameandika ujumbe huo, huku Dirisha Dogo la Usajili likitarajiwa kufunguliwa Desemba 15.

Young Africans kwa sasa inatajwa kuwa kwenye mawindo ya kurudisha nchini Kiungo kutoka nchini Zambia caltous Chota Chama na huenda andiko lake likawa linamuhusu mchezaji huyo.

Manara ameandika: Nchi tuisimamishe sasa hv au baadae? Dadadeki, Ok biashara tushamaliza na hapa Hersi @caamil_88 ndio anashughulikia ATC, oooh Tholi ni ITC

Jana mliongopewa nn vile?

We Are Yanga, The Home of Champions

Sijui nifanye Press au niseme humu humu, halaf wala haturingi

Geita Gold FC yahamia kwa Mukoko Tonombe
Simulizi: Kidogo nipoteze Mume baada ya kujifungua kwa upasuaji