Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba,Haji Manara ametoa angalizo kwa Mwenyekiti wa kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inayoshughulikia mgogoro wa mkataba wa mchezaji Bennard Morrison na Young Africans, kutenda haki la sivyo wataingia matatizoni.

Manara amemtaka mwenyekiti wa kamati hiyo Elius Mwanjala kutoa maamuzi yaliyo nyooka na kusikiliza hoja iliyo mezani inayohusisha kufojiwa kwa mkataba wa nyota huyo raia wa Ghana.

Aidha amesema Serikali ya Rais wa nchi Dokta JPM ipo macho na inafuatilia Mambo Kama haya, huku akitoa angalizo kuwa watu wakileta mzaha watafungwa kama ilivyokua kwa aliyekua Rais wa TFF Jamali Malinzi.

Manara ameongeza kuwa utawala huu sio Kama wa awamu zilizopita, Takukuru na taasisi zote zinachungulia suala hili, hivyo watu wasilete mzaha.

Serikali: maudhui ya radio za nje yapitie TCRA
Marekani: Historia mpya yaandikwa