Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kubwaga kwenye tuzo ya Muhamasishaji Bora msimu wa 2020/21.

Tuzo hiyo ilikwenda kwa Shabiki wa Taifa Stars Bongo Zozo, ambaye alishindanishwa na Manara pamoja na Masau Bwire wa klabu ya Ruvu Shooting.

Manara amefunguka kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, akimjibu Bongo Zozo ambaye amejinasibu hakustahili kutangazwa kuwa mshindi.

Bongo Zozo anaamini Manara alistahili tuzo hiyo kwa kazi kubwa ya kuwahamasisha Mashabiki aliyoifanya kwa timu ya Taifa Stars na alipokua Simba SC kabla ya kuhamia Young Africans.

Manara Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameandika: “TFF wanajua mm na ww ni marafiki na majirani hapa Dar,,ukiishi Sleep Way jirani na kwangu, ndio maana hata kadi yako ya jana ya mwaliko ililetwa kwangu,,,

“Ww kushinda hii tuzo kwangu pia ni sahihi sana coz umeshinda Mpira wa miguu,ningeshinda mm na kwa siasa za Soka letu lilivyo ingekuwa,,,,,,”

“Kongole my friend na usijali,,wengine tuzo zetu watakuja kupokea Watoto wetu tukiwa kaburini tumepumzika”

But once again Congratulations Pacha

Twiga Stars yakamilisha maandalizi
Fahamu Undani wa Bibi Titi na UWT