Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amesema kuwa hivi sasa Simba na mashabiki wake hawawezi kuwa wazalendo kwa Yanga bali uzalendo pekee watakuwa nao kwenye timu ya taifa tu.

Ameyasema hayo mara baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho huku Yanga nayo ikiwa imeondolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika. baada ya timu hizo kuondolewa kwenye michuano hiyo zote zikiwa ugenini na kutoka suluhu ya bila kufungana.

Aidha, kutokana na suluhu hiyo, mashabiki wengi walianza kutoa lawama kuwa timu hizo kwa kuwa zilishindwa kujipanga vyema na kutumia vizuri uwanja wa nyumbani.

“Naona huko mitandaoni baadhi ya wanayanga wanataja sababu mojawapo ya timu za bongo kutofanya vizuri uwanja wa nyumbani ni kukosa uzalendo kwa vilabu vyetu, wanalosahau wao nililisema hadharani mapema na nikabezwa na viongozi wao, leo ndio mwaujua uzalendo? Nawaambia kwa sasa tutafanya zaidi yenu, uzalendo wetu utabaki kwa timu za Taifa tu,”amesema Manara

Rwanda kupiga mnada mali za Diane aliyetaka kugombea urais
Mkapa: Elimu yetu ina ‘mushkeli’