Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa vinara wa Ligi Kuu (VPL) Simba SC, Haji Manara amesema kuwa nyota wa Yanga, Ibrahim Ajib ni mchezaji bora na mwenye kipaji kilichokuwa kizuri zaidi nchini huku akiwataka mashabiki wa Yanga kuacha kumtolea maneno ya fedheha mchezaji huyo.

Ameyasema hayo kupitia ukurasa wake maalum wa kijamii baada ya kuwepo taharuki kubwa kwa mashabiki wa soka wa Yanga kwa kitendo cha mchezaji huyo pamoja na wenzake watatu kutoweza kuungana na kikosi kilichosafiri juzi kuelekea nchini Algeria licha ya uongozi wa Yanga kutoa sababu zenye umuhimu wa kutoshiriki wachezaji hao.

“Ni kukosa heshima kuliko pitiliza, ni kukosa shukrani na heshima kuna kofaa kukemewa na wadau wote. Kwangu mimi Ajibu ni kipaji maridhawa zaidi nchini kilicho hai hakuna gundu wala nundu,”amesema Manara

Kwa upande mwingine, Manara amempa ushauri mzito Ibrahim Ajib kuwa endapo ataona mambo yamezidi kuwa magumu huko alipo sasa basi asisite kurudi Simba SC kwa kuwa alivyoondoka hakuua mtu yeyote aliondoka kwa amani na upendo juu yake.

 

 

Video: Wabunge upinzani wasusia bunge..., Familia yalilia haki za mbunge
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 5, 2018