Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Haji Manara mesema jambo ambalo amefanya Mshauriwa harakati za mabadiliko ndani ya Young Africans Senzo Mazingiza Mbatha la kukutana na Kocha Mkuu wa Al Ahly, Pitso Mosimane sio la kiungwana na hakupaswa kufanya hivyo.

Manara amesema kwa mtu muungwana hakupaswa kufanya hivyo kwa kuwa Simba ipo kwenye mapambano kwa ajili ya taifa la Tanzania.

“Nasikia watu wanasema kwamba alikuwa amekwenda kukutana na ‘Msauzi’ mwenzake (kwa kuwa Senzo na Misomane ni raia wa Afrika Kusini), ila ninaamini kwamba sio sawa.”

“Inaelezwa alianza kusema kwamba alitaka kuonana naye siku ya Ijumaa ila akakwama na kuamua kuchagua Jumatatu, hapana kwa nini iwe siku moja kabla ya mechi?” aliohoji Manara

“Ingekuwa yupo ndani ya Simba angeweza kufanya hivyo? Sisi huwa tunaonana nao kwa mujibu wa taratibu kwa kuwa kuna muda wa kufanya vikao kama vile kabla ya mechi hapo tunaongea na kubadilishana mawazo kwa kuwa mpira sio vita.”

“Kikubwa ninawaambia mashabiki wawe na subira unapozungumza kuhusu Simba unazungumzia taasisi kubwa yeye watu wengi, sasa tunafanya vitu vyetu kwa umakini mkubwa,” amesema.

Naye Mjumbe wa Bodi na Mshauri wa Benchi la ufundi, Crescentius Magori ameungana na Manara kwa kumlaumu Senzo kwa kitendo alichokifanya cha kukutana na kocha wa Al Ahly siku moja kabla ya mchezo.

“Hizi timu Simba na Yanga ni utamaduni wetu unapojaribu kumkandamiza Simba au Yanga katika mechi za kimataifa hausaidii soka letu.”

‘’Senzo kakosea sana, kwani angesubiri mechi iishe ndipo akutane na Mosimane kingeharibika nini ?! Anaweza kuwa hakuwa na nia mbaya, lakini nani ataamini hilo ukizingatia siasa za Simba na Yanga” amesema Magori.

Hata hivyo Magori ametoa ufafanuzi wa vita iliopo baina ya mashabiki wa klabu za Simba na Young Africans pale timu zao zinapocheza dhidi ya timu kutoka nje ya nchi, hususan kwenye michuano ya kimataifa.

Magori amesema tabia ya kushabikia timu kutoka nje ya nchi haikuwepo siku za miaka ya nyuma, lakini katika mwaka 1993 i mashabiki wa Young Afruicans ndio walioianzisha , pale Simba ilipopoteza mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Stella Abidjan kwa kufungwa mabo mawili kwa sifuri Uwanja wa Taifa ambao kwa sasa unafahamika kama Uwanja wa Uhuru.

“Yanga ndio walianza kushangilia wageni, zamani hakukuwa na tabia hiyo, kwa mara ya kwanza mashabiki wa Tanzania kushabikia vilabu vya nje ngazi ya vilabu ilianza mwaka (1993) katika fainali ya (CAF) wanaYanga walipoona tumeruhusu bao la pili, waliimba, “UZALENDO UMETUSHINDA” , na ikukmbukwe kuwa kabla ya hapo Simba hatukuwahi kuziunga mkono timu pinzani hata siku moja” ‘’

“Mimi nilishawahi kuwa kiongozi (CECAFA) nk .. najuana na viongozi wengi, lakini ulishaniona hata siku moja naongea na wapinzani wanaokuja kucheza na Yanga ? Kwani Senzo angemtafuta kocha wa Al Ahly kwa njia ya Simu kungekuwa na tatizo?” amesema Magori.

Young Africans yaiandalia 'DOZI' Kengold
CAF yaitengea Namungo FC Mil 635