Kati kati ya juma lililopita zilienea habari katika mitandao ya kijamii kuwa Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa MeTL Group, Mohammed Dewji na Yusuph Manji wote kwa pamoja wamesitisha mipango ya kuwekeza katika klabu za Simba na Yanga.

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kwa upande Simba jinsi ambavyo wamelipokea jambo hilo, na kusistiza halina ukweli kwani kila kitu kinaendelea kama kilivyopangwa.

“Nimesikia hizo taarifa na kazi kubwa ya mitandao ya kijamii siku hizi ni kupotosha, hazipo official (rasmi) sisi kama klabu … ninavyoamini mimi hizo taarifa hazipo kwetu na sichukulii kwa uzito wowote,” alisema Manara.

Aidha amezungumza kuhusu agizo la serikali kuwazuia kufanya mabadiliko ya kimfumo ambayo yatamwezesha MO Dewji kuwekeza na kusema kuwa wao wameshapata ridhaa ya wanachama na utaratibu wa kufanya mabadiliko unaendelea.

“Serikali haikatai mabadiliko, imetoa agizo kuwa michakato hii ifate taratibu ikiwepo mabadiliko ya kikatiba ambayo klabu ya Simba imezingatia, tumeita mkutano wa wanachama na wamesema wanataka kuingia katika mabadiliko na sisi hatuna presha na hata MO hana presha,” alisema.

“oon tutatoa taarifa rasmi namna mchakato huu utakavyofanikiwa kwa kuzingatia katiba ya Simba, katiba ya nchi na kanuni na sheria zinazosimamia mpira wa miguu, hatuna pressure yoyote,” alisema Manara.

Rais Wa Armenia Ashindwa Kumuelewa Mourinho
Faraja Kotta aumizwa na kinachomkuta Miss Tanzania Mpya, akumbuka machungu