Wakati wadau wa soka wakisubiri aombe radhi ndani ya siku 14 alizopewa na uongozi wa Young Africans, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Manara kwa mara ya kwanza amajiapiza kutokutoa maneno ya utani.

Young Africans kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Fredrick Mwakelebela walimtaka Haji Manara kuomba radhi ndani ya siku 14, kwa kosa la kuidhihaki Brand ya klabu hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, na kinyume na hapo watamfikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Manara amejiapiza kutokutoa maneno ya utani dhidi ya Young Africans alipohojiwa na kwenye kituo cha Wasafi FM kupitia kipindi cha Sports Arena mapema hii leo (Jumatatu, Februari 22).

Manara amesema: “Unajua katika vitu ambavyo Mimi Huwa sichukizwi navyo ni kuhusu utani wa Simba na Yanga mtu anaweza kunitania nikachukulia ni katika Ushabiki tu, Lakini Hawa wenzetu ukiongea kidogo tu wanakuja juu.”

“Miaka ya Nyuma wao walikuwa Wanafanya vizuri Sana Kwenye Ligi Simba ikiwa vibaya, walikuwa wakitutania Sana na kututupia Maneno ya kila aina lakini Sasa Hivi Wao ukisema kidogo tu Maneno mengi, Sasa kuanzia leo hutoniona naitania Yanga.”

Majaliwa awakabidhi magari polisi Lindi
Simba SC, Namungo FC kuinufaisha Tanzania 2021/22