Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Ramadhan Manara, amethibitisha kuhojiwa na Televisheni ya Taifa ya DR Congo, kuelekea mchezo wa kwanza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba SC, itacheza dhidi ya AS Vita Club mjini Kinshasa kesho Ijumaa, na tayari imeshawasili mjini humo tangu jana, ambapo ilifanya mazoezi yake ya kwanza kwenye uwanja wa De Martyrs (Stade De Martyrs).

Manara amethibitisha kuhojiwa na kituo hicho cha taifa cha DR Congo kwa kuandika taarifa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii (Facebook na Instagram).

Manara ameandika: “Tulichowaambia TV ya Taifa ya Congo ni kwamba, Simba inawaheshimu Vitta Club na inajua ni ngumu mno kucheza nao kwao kisha kupata matokeo chanya,lakini hatukuja huku kumuogopa mtu!!”

“Heshma yetu ni ya kimchezo na hatuiangalii historia ya mechi iliyopita ya hapa Kinshasa,”

“Kocha wetu ni mwerevu na atakuja na plan sahihi ya kucheza away game kama hz!!”

“Shida kubwa nnayoiona  ni kwangu binafsi,,inanibidi kuongea lugha za kifaransa na kilingala kila wakati,,Dua zenu ndugu zangu,”,

“Mashavu yangu yapo taabani.”

Mungu ibariki Simba

Mungu ibariki Tanzania

@hajismanara

Majaliwa afafanua nyongeza ya mishahara
CORONA: CAF yafanya mabadiliko