Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Ramadhan Manara amewahakikishia mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kila kitu kipo salama huko nchini Sudan, walipokwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi dhidi ya Al Merrikh.

Simba SC iliwasili mjini Khartoum usiku wa kuamkia jana Alhamis (Machi 04), na tayari imeanza mazoezi rasmi katika uwanja wa Jeshi mjini Khartoum, huku kila mchezaji akionesha utayari wa kuelekea mpambano huo utakaochezwa kesho Jumamosi (Machi 06).

Manara amesema hali ya wachezaji ipo salama na anaamini kilichotokea mjini Kinshasa, DR Congo kwa kuibanjua AS Vita Club na kisha jijini Dar es salaam kwa kuifunga Al Ahly, huenda kikatokea mbele ya Al Merrikh kesho Jumamosi.

Pia amewataka mashabiki na wanachama wa Simba SC sambamba na watanzania kwa ujumla kuiombea Kheir timu ya Simba SC ambayo inajukumu la kuiwakikisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

“Kikosi kipo tayari, tumekuja hapa kupambana tunaamini kila mmoja atabeba hiyo dhana ya mapambano, In Shaa Allah tutafanikisha hilo ndani ya dakika 90.”

“Tunawaheshimu wenyeji wetu, waka kikosi kizuri na wana uzoefu mubwa katika michuano ya Afrika, lakini hatukuja hapa kufurahishana wana kutishana, tumekuja kupambana.”

“Jambo kubwa na muhimu kwa kila mtanzania ni kunyanyua mikono kutuombea dua ili tufanikiwe kufanya vizuri katika mchezo wetu wa kesho Jumamosi,”

“Ninaamini tukiwa kitu kimoja na kila mmoja akaeleza dua zake kwa M.Mngu, hakuna litakaloshindikana In Shaa Allah.” Amesema Manara

Simba SC inaongoza msimamo wa ‘KUNDI A’ kwa kufiksha alama 6, baada ya kuzifunga AS Vita Club na Al Ahly, huku mpinzani wake wa kesho Al Merrekh waiburuza mkia wa kundi hilo, kufutia kufungwa michezo miwili iliopita.

Katwila, Anuary Jabir wang'ara Ligi Kuu
Wadada, Sebo kuikosa Mwadui FC