Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS) imepanga kutangaza maamuzi ya pingamizi la mabingwa wa soka England (Manchester City) juu ya kifungo cha kutoshiriki michuano ya Barani Ulaya (UEFA Champions League na Europa League) kwa misimu miwili mfululizo.

Wanasheria wa Mahakama hiyo watatoa maamuzi yao baada ya kukaa kikao kwa njia ya video kwa siku tatu wakijadili pingamizi ambalo liliwasilishwa na klabu ya Manchester City.

“Pande zote mbili zimetoa utetezi wao, ambapo kila hatua ya usawa ilizingatia yamebaki maamuzi ya mahakama hiyo”.

Mwezi wa Februari tarehe 14, Bodi ya Usimamizi wa Matumizi ya Fedha (CFCB) iliifungia klabu hiyo na kuwapiga faini ya Euro milioni 30 baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni matumizi ya fedha na kuvunja kanuni za FFP.

Hata hivyo, CFCB ilisema Manchester City hawakutoa ushirikiano wa kutosha kwa Bodi hiyo kati ya mwaka 2012 – 2016 kipindi cha uchunguzi.

Mdee na Bulaya watua Takukuru
Magufuli: Tusidharau dawa za kienyeji "Uchawi ndiyo mbaya"