Klabu ya Manchester United ndio klabu yenye thamani kubwa kuliko zote barani Ulaya ikiwa na thamani ya Euro bilioni 3 kufuatia utafiti uliofanywa na kampuni ya biashara ya KPMG.

Aidha, Mabingwa hao wa kombe la Europa wanaongoza katika orodha hiyo ya thamani ya Kampuni ya KPMG, ikiwa mbele ya mabingwa wa Hispania, Real Madrid na Barcelona.

Katika Utafiti huo uliofanywa na kampuni hiyo vigezo vya msingi vilivyotumika ni pamoja na urushaji wa matangazo, faida, umaarufu, uwezo kimchezo na umiliki wa uwanja,huku kukiimarika kwa matangazo, operesheni za biashara za kimataifa, uwekezaji wa vifaa vya umiliki wa kibinafsi, vifaa vya kisasa pamoja na usimamizi mzuri ni vigezo muhimu vya ukuaji huo.

Dar24 imekuandalia orodha ya Vilabu kumi bora vyenye thamani ya juu kibiashara

1.Manchester United -Euro 3.09bn

2.Real Madrid – Euro 2.97bn

3.Barcelona – Eur o2.76bn

4.Bayern Munich – Euro 2.44bn

5.Manchester City – Euro 1.97bn

6.Arsenal – Euro 1.95bn

7.Chelsea – Euro 1.59bn

8.Liverpool – Euro 1.33bn

9.Juventus – Euro 1.21bn

9.Tottenham – Euro 1.01bn

10.Duru: KPMG

Idris Sultan awapa ‘neno’ wanaopost iftari zao mitandaoni
Bunge nchini Marekani lataka wakili wa Trump ahojiwe