Klabu ya Manchester United itacheza na mahasimu wake Manchester City katika mchezo ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi ya England kupitia michuano ya International Champions Cup itakayofanyika mwezi Julai.

Mahasimu hao ambao walishindwa kukutana katika michuano hiyo mwezi Julai mwaka jana huko China kufuatia uwanja wa kiota cha ndege uliopo mjini Beijing-China kuharibiwa na hali ya hewa kwenye sehemu ya kuchezea.

Mbali na Man City, Man utd pia itacheza na Real Madrid na Barcelona, katika michuano hiyo amayo itafanyika nchini Marekani, China na Singapore.

Ratiba ya michuano hiyo ilitolewa jana na kuonyesha klabu nyingine ya England  Tottenham Hotspurs itashiriki michuano hiyo, na mchezo wake wa kwanza itapambana na Man City Julai 29 kwenye  uwanja wa Nissan uliopo mjini Nashville.

Barcelona na Real Madrid watapambana nje ya Hispania kupitia michuano ya ICC katika mji wa Miami Julai 29 kwenye uwanja wa Hard Rock.

Man Utd itacheza na miamba hiyo ya La Liga, ambapo itaanza na Real Madrid Julai 23 na kisha FC Barcelona Julai 26.

Timu nyingine zitakazoshiriki ni Paris St Germain AS Roma Juventus, Inter Milan, Borussia Dortmund, Bayern Munich, Arsenal, Chelsea na Atletico Madrid.

Katika kundi la Marekani kutakua na timu za Paris Saint-Germain, FC Barcelona,  Real Madrid, Manchester United, Manchester City, Tottenham Hotspur,AS  Roma na  Juventus.

Kundi la China: A.C. Milan, Borussia Dortmund  Dortmund, Bayern Munich na Arsenal.

Kundi la Singapore: Inter Milan, FC Bayern Munich na Chelsea

Gary Cahill Kuiongoza England Dhidi Ya Ujerumani
Ozil, Draxler, Gomez Kuikosa England